Saturday, June 9, 2012

Je! Na wewe ulikuwepo huko…?


Uhai ni zawadi ya pekee kutoka kwa Mungu. Wototo ni majaliwa ya Mungu. Kwahiyo ni wazi kuwa, watoto ni zawadi ya pekee kutoka kwa Mungu. Tunaona ni jinsi gani watu wanavyotafuta watoto, katika mazingira ambayo tumekutana nao, na hata hivyo katika biblia tunasoma na kuthibitisha ukweli huu. Tunaona Sarai mkewe Abrahamu alikosa mtoto na alikuja kupata  badaye mtoto wa pekee  Isaka.  Tunamuona Rahel na hadith yake inafanana na hiyo, na wengine wengi. Si hao tu katika biblia, bali hii ni hali  halisi pia katika mazingira tunamoishi. Lakini chakushangaza tunaona wengi wanapingana na zawadi hii (bila huruma), tukianza na herode, alivyo jaribu kumuangamiza Yesu, na baadaye akawauwa watoto wengine wengi. pia. Katika jamii ya sasa kuna wale wanao watelekeza watoto wao,  pia wanaowatupa majalalani watoto wao nk.
Kuna tafsiri mbalimbali mbali juu ya mtoto ni nani? Lakini, leo tutashirikiana kuwatazama, binadamu waadilifu wasiozidi miaka kumi. Ninamaanisha tupo huru kuwazungumzia wale wenye miaka sufuri hadi hicho kikomo nilichotaja.
 Nimevutiwa kuandika kifungu hiki kwa sababu ya  hazina kubwa iliyo ndani ya watoto wetu. Pia malezi wanayopata watoto yanamchango mkubwa katika kuandaa watu wa baadaye (hasa kisaikologia na Nyanja zinginezo). Waswahili husema “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.” Kumbe basi, tukiwalea watoto hawa katika mazingira ya maadili mema, ndivyo watu wa kisho watakavyo kuwa waadilifu; watakuwa wema na msaada katika jamii yote kwa ujumla. Lakini wakilelewa katika mazingira ya kikatili, kifisadi, kiwazi, n.k., ndivyo    watakavyo jiimarisha kwa tabia hizo yaani, makatili, mafisadi, wezi, kujumulisha sugu.  Na hii haipingiki kuwa ni hasara kwa wazazi na jamii kwa ujumla.

Tofauti katika uwezo mbalimbali kijinsia
Tofauti hizi ni kutokana na wataalamu mbalimbali waliofanikiwa kuchunguza tabia mbalimbali juu ya jinsia mbili na kwa wakati huu hasa kwa watoto wadogo ambao baadaye, kwa matumaini watakuwa watu wa umri wa utu uzima. Na hatimaye tofauti hizi hazi lengi katika kuwagombanisha au kutafuta nani anafaa zaidi, bali ni katika kusaidia kuleana na kuboresha ubinadamu wetu, kwa kadiri ya makusudi ya mungu.
Kuona, watoto wakike wanauwezo wakuona zaidi karibu kuliko wa kiume. Ndio maana takwimu zinaonesha kuwa, ajali za barabarani hasa zinazowahusu watoto wadogo; idadi ya watoto wa kiume ni zaidi ya wale wa kike.Hivyo, wazazi, walezi na jamii yote kwa ujumla ni vema wakafahamu hilo kisha waelekeza maarifa yao katika kuwasaidia kwa kadiri ya mahitaji.
Kusikia, inasemekana kuwa watoto wakike ni wapesi kusikia kuliko wa kiume. Ndio maana husemwa kuwa, mtoto wakike kwa umri wa wiki moja anaweza kutofautisha sauti ya mama yake na sauti za watoto wengine wakilia. Kitu ambacho ni mtihani kwa mtoto wa kiume.
Kuongea, watoto wakike wanakuza uwezo wakuongea zaidi kuliko wa kiume. Ndio maana husemwa kuwa, jinsia ya kiume inahitaji wastani wa maneno 700 ya kuwasiliana kwa siku wakati jinsia ya kike wanahitaji wastani wa maneno 20,000 kwa siku.
Kuwanyamazisha, tofauti hii inaendana na hiyo hapo juu. Watoto wakike wakilia hunyamazishwa kwa kukuimbiwa ikikululu. Wakati watoto wa kiume, hunyamazishwa kwa kuwaongelesha au kwa michezo mbalimbali. Kuna hadithi iliyo mshusha nyoka mtini akitamani kumsahihisha binadamu iliyekosea katika ugawaji. (huyu binadamu alimpa mbwa wake nyasi na mbuzi wake nyama na mifupa. Wakati huohuo akiwa amewafunga kamba mbali mbali ili wasiingiliane katika mgawanyo huo). Bilashaka hata wewe ungetelemka mtini ili usahihishe mgawanyo huo.  Hivyo tuwasadie bila kukosea nani ni nani na anahitaji nini katika mda na wakati ufaao.
 Pia, watoto wa kike wanapenda watu zaidi wakati wale wakiume wanapenda vitu.  Ndio maana watoto wa kike huzichukulia fimwanansensere (toys) kama marafiki. Na hivyo watoto wakike huweza kutazama na kutofautisha sura za watu wa familia na wageni katika umri wa wiki kumi na mbili wakati jambo hili ni kitendawili kwa watoto wa kiume.

Maendeleo ya ki-akili
Kama ilivyo kukua pia maendeleo ya akili hukua hatua kwa hatua. Hebu tazama pia majibu wanayotoa kwa maswali mbalimbali kwa watoto wanaoweza kuongea au kujieleza. Familia inapatikana wapi? wengine husema nyumbani, wengine  husema mbinguni, wengine husema kanisani, haya yote ni majibu sahihi hasa kwao kutokana na malezi na mazingira yanayo wazunguka. Swali jingine familia ina watu gani? Wengine husema (baba na mama), wengine husema (bibi na babu), wengine ni (mjomba na wifi), wengine walisema ni (baba, mama, kaka, dada na mtoto). Chakufurahisha ni kuwa majibu ya watoto hawa hayako mbali sana na uhalisia. Yaani yanategemea sana mafundisho wanayopata na mazingira wanayoishi. Hivyo si ajabu katika swali “Kazi ya baba ni nini?” kupata majibu yafuatayo: kunywa pombe (kulewa), wengine kuleta mahitaji, kulima, kwanda kazini, na wengine, kugombeza familia, kuadhibu watoto vikali wanapokosea, kuchelewa kuja nyumbani. Majibu haya yote yanawaza kuwa si sahihi katika mitihani ya darasani,
 lakini yana usahihi wake katika halihalisi ya maisha kwa kuwa yanaakisi na kusadifu mazingira halisia. Pia kondoo ni nini? Ni mbuzi?  linaweza kuwa ni jibu kwa swali hili.
                 Ndugu msomaji waswahili husema “Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu…?” ni rahisi kuuliza na kupata majibu. Hapa ndipo kipima joto kilibadili uelekeo. Kama umezoea kuuliza basi tuone wewe unajibuje? Mimi niliuzwa swali na mdogo   wangu, ndio nikasikilizia joto lake!! Swali liliulizwa kwa heshima kabisa, kwamba kaka “Je vifaranga vikifa vinaenda mbinguni…..?”
Kuhusu mawazo mengine watoto wanamitazamo ifuatayo. Kuhusu maisha (life), kwao kila chenye mwendo kina uhai, hivyo hata gari lina uhai. Kuhusu kifo wengine wanafikiri kuwa si kitu cha kudumu. Hivyo wanaweza kuuliza, kwa nini waliokufa hawarudi? Uzito kwao ni sawa na ujazo, mfano debe moja la manyoya kwao lina uzito sawa na debe moja la mahindi. Wanaweza kuelewa namba 1-5, zaidi ya hapo, wanahesabu tu bila kuelewa. Kuhusu muda hawawezi kutofautisha usiku na mchana. Hawawezi kutofautisha wiki, siku saa nk. Mfano sentensi “Nilikuja kesho na nitakuja jana” zinaweza kuwa sahihi kwao.  Kwa sababu ya uhaba wa nafasi naomba kwa leo niishie hapa. Ni ushauri wangu kuwa tuwapende watoto wetu, tuwatunze watoto wetu, na tuwalee vizuri watoto wetu. maana ni tumaini la kanisa na pia ni taifa la kesho, bila kusahau mchango wao leo. Mungu na atubariki na kutuangazia uso wake.



No comments:

Post a Comment